Nyimbo za wokovu
Wimbo 176 Kutoka Dhambini Maneno ya wimbo
Kutoka dhambini mpaka mbingu,
nimeshikwa na pendo la Mungu;
Kwa vifungoni nimeondoka,
Na Yesu hunishika.
Yesu hunishika,
Yesu hunishika;
Kutoka gizani mpaka mwanga,
Na Yesu hunishika.
Kutoka taabu mpaka raha,
Nimefika nchi ya Baraka;
Kwa fahari yake nitakaa,
Na Yesu hunishika.
Kwa kujitoa nitamwabudu,
Kwa pendo lake nitamshukuru;
Kwa milele naye nitakaa,
Na Yesu hunishika.