Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 162 TUMAINI LIKO nyimbo za wokovu
1
Tumaini liko
La thamani kuu,
Kupita anasa tupu
Zake ulimwengu.
2
Pana nyota nzuri:
Nuru itoayo
Kwetu wakati wa kifo
Ndio ufufuo.
3
Zikiumwa roho
Na hofu, mashaka,
Sauti hutuambia
Mungu hutupenda.
4
Kutoka Kalwari
Sauti hunena;
Nyota ni nuru ya mbingu,
Tumaini letu.