Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 154 YANIPASA KUWA NAYE nyimbo za wokovu
1
Yanipasa Kuwa naye
Mwokozi Bwana wangu,
Akiwa karibu nami,
Napata nguvu kweli.
Moyo hauogopi,
Wala kutikisika.
Nitakwenda apendapo,
Kwa kuwa anilinda.
2
Yanipasakuwa naye,
Kwani nategemea;
Anaweza kufariji
Na maneno matamu.
3
Yanipasa kuwa naye
Maisha yangu yote;
Yakiwapo majaribu
Na mashaka yo yote.
4
Yanipasa kuwa naye
Katika njia zangu;
Macho yake yaongoza
Hatua zangu zote.