Nyimbo Za Sifa
Wimbo 72 Sioni Haya kwa Bwana. Maneno ya wimbo
Sioni haya kwa Bwana
Kwake nitang’ara’
mti wake sitakana
Ni neno imara!
Chorus
Msalaba ndio asili ya mema
Nikatua mzigo hapo
Nina uzima, furaha daima
Njioni kufurahini papo
Kama kiti chake vivyo
Ni yake ahadi
Alivyowekewa navyo
Kamwe, havirudi
Bwana wangu, tena Mungu
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu
Wala kunikana
Atakiri Iangu jina
Mbele za Babaye
Anipe pahali tena
Mbinguni nikae