Nyimbo Za Sifa
Wimbo 136 Enzi lliyo juu. Maneno ya wimbo
“Enzi iliyo juu
Na nchi amani”
Punde zitakwisha
Zani za vitani
Amezawa Mkombozi
Bethilehemu, sifuni
Ni tunu ya kweli
Mwokozi i mkuu
Kila ukaidi
Na nguvu zake kuu
Kwako hwishia, ndiposa
Twakuamini kabisa
Mungu, waridhia
Mwana wa Adamu
Kwake zako njia
Zaonywa timamu
Huyo ni Mpenzi wako
Na chombo cha sifa zako
Uzao wa mke
Ni Bwana wa enzi
Mwana-Mungu pweke
Yu pweke mtenzi
Sifa waimbazo wa juu
Ni zako Wewe jesu tu
Tusiposhukuru
Mawe yatalia
Heri tumwabudu
Na kushangiria
Bora, Bwana, kazi zako
Hutwonya wokofu wako
Enzi iliyo juu
Tunaimba nasi
Ndako ibada kuu
lsiyo kiasi
“Amani hata Mbinguni”
Ulipo Yesu enzini