Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 60 NITAKWENDA UTAKAPONITUMA nyimbo za wokovu
1
Pengine siyo milimani
Utakaponiita;
Pengine siyo baharini
Wala palipo vita;
Lakini unaponiita,
Na njia siijui.
Bwana, nitajibu,
ni tayari Kwenda uniagizapo.
Ukiwa pamoja nami,
Bwana, Mlimani, baharini,
Niende utakaponiita;
Na fuata uendako.
2
Pengine leo kuna neno,
Neno tamu la pendo,
Ambalo Yesu anataka
Ninene kwa upole;
Ukiwa pamoja nami,
Bwana, Nitamtafuta leo
Yule aliyepotea mbali:
Nitasema upendavyo.
3
Pahali pako bila shaka
Pa kuvuna shambani,
Kazi niwezayo kufanya
Kwa Yesu Mkombozi;
Hivi nikikutegemea,
Kwa kuwa wanipenda,
Mapenzi yako nitayafanya,
Na niwe upendavyo.