Nyimbo za wokovu
Wimbo 96 Wamwendea Yesu? Maneno ya wimbo
Wamwendea Yesu kwa kusafiwa,
Na kuoshwa kwa damu ya Kondoo?
Je, neema yake yatumwagiza?
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?
Kuoshwa, kwa damu
Itutakasayo ya Kondoo?
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?
Wamwandama daima Mkombozi
Na kuoshwa kwa damu ya Kondoo?
Yako kwa Msulubiwa makazi?
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo.
Atakapo kuja Bwana-arusi
Uwe safi kwa damu ya Kondoo:
Yafae kwenda Mbinguni mavazi
Yafuliwe kwa damu ya Kondoo.
Yatupwe yaliyo na takataka,
Na uoshwe kwa damu ya Kondoo?
Huoni kijito cha tiririka
Na uoshwe kwa damu ya Kondoo.