Nyimbo za wokovu
Wimbo 91 Mkuu Akamjia Yesu Usiku Maneno ya wimbo
Mkuu alimjia Yesu usiku,
Kwa kumwuliza njia ya wokovu;
Kwa udhahiri akamjibu Bwana,
Uzaliwe tena.
Uzaliwe tena,
Uzaliwe tena;
Amini, Amini, nakuambia
Uzaliwe tena.
Sikilizeni, Enyi wanadamu,
Na lishikeni Neno lake tamu;
Jinsi Yesu kwako alivyonena,
Uzaliwe tena.
Enyi mtakaoingia raha,
Kuimba na waliokombolewa;
Ukipate kipawa cha uzima,
Uzaliwe tena.
Mpendwa wako aliye mbinguni,
Atakukaribisha mlangoni;
Uyasikie maneno ya Bwana,
Uzaliwe tena.