Nyimbo za wokovu
Wimbo 67 Tafuta Daima Utakatifu Maneno ya wimbo
Tafuta daima utakatifu,
Fanya urafiki na Wakristo tu;
Nena siku zote na Bwana wako,
Baraka uombe kwa kila jambo.
Tafuta daima utakatifu,
Uwe peke yako ukimwabudu;
Ukimwangalia Mwokozi wako,
Utabadilishwa kama alivyo.
Tafuta daima utakatifu,
Kiongozi wako awe Yesu tu;
Katika furaha au huzuni,
Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.
Tafuta daima utakatifu,
Umtawaze Roho moyoni mwako;
Akikuongoza katika haki,
Hufanywa tayari kwa kazi yake.