Nyimbo za wokovu
Wimbo 52 Nina Furaha Kazini Maneno ya wimbo
Nina furaha kazini mwa Yesu,
Nafurahi, nafurahi;
Nina amani iliyotoka juu,
Kumtumikia Yesu.
Kumtumikia Yesu,
Nimevileta vyangu;
Nina amani na furaha
Kazini mwa Yesu.
Nina furaha kazini mwa Yesu,
Nafurahi, nafurahi;
Ijapokuwa shaka na taabu,
Nitamhudumu Yesu.
Nina furaha kazini mwa Yesu,
Nafurahi, nafurahi;
Nitamshika nipate kufaulu,
Kumtumikia Yesu.