Nyimbo za wokovu
Wimbo 211 Katika Gethsemane Yesu Aliteswa Maneno ya wimbo
Katika Gethsemane Yesu aliteswa,
Kikombe chenye huzuni, hapo alikunywa;
Pa Kalvari, Msalabani aliuchukua,
Alitenda mapenzi ya Baba.
Pekee, ndiyo pekee, Yesu alikufa,
Pekee, ndiyo pekee alinifungua;
Dunia hii iliaibishwa hata Yesu
Alitenda mapenzi ya Baba.
Yesu alikubali kunifia mtini,
Akamwaga damu yake nisife dhambini;
Akawekwa katika kabirini mwambani,
Alitenda mapenzi ya Baba.
Alifufuka kutoka kifo na kaburi,
Akawa Mshindi juu ya mauti na dhambi;
Akaniokoa nisiende hukumuni,
Alitenda mapenzi ya Baba.