Nyimbo za wokovu
Wimbo 190 Siku Nilipokuwa Dhambini Maneno ya wimbo
Siku nilipokuwa dhambini,
Nikaambiwa juu ya Mwokozi;
Nikasikiliza na furaha,
Kufahamu kwamba nitaokoka.
Niliambiwa Yesu apenda,
Aliyenifia Msalaba;
Dhambi zangu ataziondoa,
Nikaambiwa Yesu apenda.
Tangu nilipoonja upendo,
Yesu hukaa ndani ya moyo;
Humu dunia ni kama mbingu,
Kwani Kumjua Mwokozi ni tamu.
Ili kazi nimfanyie Bwana;
Maneno hayo ninayataja,
Ninatembea pamoja naye,
Hapo ndipo furaha siku zote.