Nyimbo za wokovu
Wimbo 170 Ni Mali Ya Mfalme Maneno ya wimbo
Ni mali ya Mfalme,
Ndimi mwana wake,
Nitakaa mahali pake,
Hapana huzuni, ni raha mbinguni,
Watu wake wataurithi.
Ni mali ya Mfalme,
Kwa upendo wake,
Na hatawaacha wenzake;
Nitaitwa naye kwa kuishi pake,
Niwe karibu enzi yake.
Ni mali ya Mfalme,
Najua ni wake,
Na neema ni ya thamani;
Napata hisani kwenda na imani,
Kimbilio langu ni Yesu.
Ni mali ya Mfalme,
Na ahadi zake,
Atazitimiza kabisa;
Nitakwenda naye mbinguni mwake,
Sitaziona shaka kamwe.