Nyimbo za wokovu
Wimbo 100 Deni Yangu Ya Dhambi Maneno ya wimbo
Deni yangu ya dhambi,
Yesu amelipa;
Kwake Msalabani
Nilipewa uzima.
Deni ya dhambi,
Msalabani;
Ilimalizikia
Ni huru kabisa.
Bwana Yesu asema,
Mwanangu dhaifu,
Uwezo na ushindi,
Hupatikana kwangu.
Bwana, kweli naona,
Nguvu zako pekee;
Huondoa ukoma,
Niwe kipya kiumbe.
Sina wema moyoni;
Nidai neema;
Nakubali kabisa,
Kwa damu kusafiwa.
Hata huko Mbinguni,
Miguuni pake;
Yesu alinifia,
Nitaimba milele.