Nyimbo Za Sifa
Wimbo 44 Twae Wangu Uzima. Maneno ya wimbo
Twae wangu uzima
Sadaka ya daima
Twae saa na siku
Zikutukuze huku
Twae mikono nayo
lfanye upendavyo
Twae yangu miguu
Kwa wongozi wako tu
Twae sauti yangu
Niimbe kwa Mungu tu
ltwae na midomo
Ijae neno lako
Twae dhahabu pia
Na yote ya dunia
Twao yangu hekima
Upendavyo tumia
Nia itwae, Mungu
Haitakuwa yangu
Twae moyo, ni wako
Uwe makazi yako
Twae mapenzi yangu
Sifa za moyo wangu
Twae kabisa nafsi
Niwe wako halisi