Nyimbo Za Sifa
Wimbo 151 Leo Yesu Kristo Amefufuka. Maneno ya wimbo
Leo Yesu Kristo amefufuka
Kifo kimeshindwa; furahi mbingu
Aleyeuawa amefufuka
Naye kwa viumbe ametukuka
Chorus
Leo Yesu Kristo, aliyekufa
Ameshinda kifo, akafufuka
Nchi yetu nayo yafurahishwa
Kwa mvua ya mbingu yaburudishwa
Mti yatepuza ya mwaka mpya
Yatuhubiri ya maisha mapya
Mwokozi, Muhui na Mumba wetu
Umeutazama uovu wetu
Wake Mungu Baba pekeo Mwana
Ulitwaa mwili nasi tu wana
Shinda Ia uzima ndiwe, ukafa
Hi sis wafu tushinde kufa
Ndiwe mwaminifu, kweli kunena
Ulivyofufuka U hai tena
Ifungue myoyo iliyofungwa
Na wakaribie waliotengwa
Twonye uso wako ujifunue
Mchana tarudi pamoja nawe