Nyimbo Za Sifa
Wimbo 146 Mungu wa Betheli. Maneno ya wimbo
Mungu wa Betheli, wewe
Uliyewachunga
Baba zetu, iwa kwetu
Chini tukitanga
Haja zetu na nadhiri
Zije kwako mbele
Kwa wazazi hata kwetu
U Mungu yeyule
Njia yote ya safari
lwa Kiongonzi
Tupe kande ya kutosha
Tupe na mavazi
Tweneze mabawa yako
Hata twishe kwenda
Ukatufishe kwa Baba
Aliyetupenda