Nyimbo Za Sifa
Wimbo 137 Ni Usiku wa Manane,Wimbo Mbinguni Unatoka. Maneno ya wimbo
Ni usiku wa manane
Wimbo mbinguni unatoka
Wimbo huo ni mzuri
Uimbwao na malaika
Chorus
Utukufu juu mbinguni
Duniani mapenzi mema!
Siku zote tutaimba
Ndiye habari njema.
Na wachunga walihofu
Wakiuona utukufu
Wakalisikia neno
La wajumbe wamemetufu
Utukufu juu mbinguni
Duniani mapenzi mema!
Siku zote tutaimba
Ndiye habari njema.
Wakaja Bethilehemu
Wapate kumsujudia
Ndiye Kristo ameshuka
Deni letu kutulipia
Utukufu juu mbinguni
Duniani mapenzi mema!
Siku zote tutaimba
Ndiye habari njema.
Mtu wa majonzi huyu
Na kukataliwa na watu
Ni Kondoo wake Mungu
Naye ndiye Mwokozi wetu
Utukufu juu mbinguni
Duniani mapenzi mema!
Siku zote tutaimba
Ndiye habari njema.