Nyimbo Za Sifa
Wimbo 122 Piga Sana Vita Vyema. Maneno ya wimbo
Piga sana vita vyema
Kwa ushujaa daima,
Yesu ndiye nguvu zako,
Yesu ndiye kweli yako.
Kaza mwendo, ushindane
Angaza macho, umwone;
Yesu ndiye njia yako.
Naye ndiye tuzo Iako.
Tupa kizito; simama,
Tazama mbele, si nyuma,
Ni Yeye uzima wako,
Naye ni kipendo chako.
Tangamka, uamini
Akashika mikononi,
Hageuki, akupenda,
Kuwa naye una pia.