Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 98 NILIKUPA WEWE nyimbo za wokovu
1
Nilikupa wewe,
Damu ya moyoni,
Ili wokolewe,
Winuke ufuni.
Nimekunyima ni wewe?
Umenipa nini?
Nimekunyima ni wewe?
Umenipa nini?
2
Nilikupa miyaka
Yangu duniani;
Upate inuka,
Kuishi mbinguni.
3
Nimekuletea,
Huku duniani;
Pendo na wokovu,
Zatoka mbinguni.
4
Nipe siku zako,
Hudumu mwangani;
Na taabu yako,
Wingie rahani.
Nafsi, nafsi, pendo, mali,
Twae Imanweli.
Nafsi, nafsi, pendo, mali,
Twae Imanweli.