Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 9 MWUMBAJI, MFALME nyimbo za wokovu
1
Mwumbaji mfalme
Vitu vyote vyako,
Ni kwa ukarimu wako
Ninabarikiwa,
Ni kwa ukarimu wako
Ninabarikiwa.
2
Uliyeniumba
Nakutegemea,
Sina budi kuzisifu
Hisani zako kuu,
Sina budi kuzisifu
Hisani zako kuu.
3
Nitatoa nini kwanza
Vyote vyako.
Upendo wako wadai
Moyo wa shukrani,
Upendo wako wadai
Moyo wa shukrani.
4
Nipewe neema
Niwe na uwezo,
Wakuishi kwako Bwana
Siku zangu zako,
Wakuishi kwako Bwana
Siku zangu zako.