Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 86 UKARIBIE TENA nyimbo za wokovu
1
Ukaribie tena,
Ewe siku ya raha;
Roho yakusalimu
Kama mwanga wa mbingu.
2
Raha yako tulivu,
Yafurahisha moyo;
Yatuliza taabu,
Hata waisha mwendo.
3
Ee siku takatifu,
Ya sifa na maombi,
Na kutuhekimisha,
Baraka yako kubwa.