Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 200 BABA YETU ALIYE MBINGUNI nyimbo za wokovu
1
Baba yetu aliye mbinguni,
Amenifurahisha yakini;
Kuniambia mwake Chuoni;
Ya kuwa nami Yesu pendoni.
Anipeda, Mwokozi Yesu,
Anipenda, Anipenda:
Anipenda, Mwokozi Yesu,
Anipenda mimi.
2
Nimuachapo kutanga mbali,
Yeye yu vivyo, hupenda kweli:
Hunirejeza kwake moyoni,
Kweli yu nami Yesu pendoni.
3
Anipenda! Nami ninampenda,
Kwa wokovu alionitenda;
Akanifilia Msalabani,
Kwa kuwa nami Yesu pendoni.