Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 166 FURAHA KWA ULIMWENGU nyimbo za wokovu
1
Furaha kwa ulimwengu,
Bwana atakuja!
Kila moyo umpokee,
Viumbe imbeni,
Viumbe imbeni,
Viumbe vyote imbeni.
2
Na Bwana atatawala;
Watu na waimbe;
Miti, milima na mawe
Kariri furaha,
Kariri furaha,
Kariri furaha kubwa.
3
Atatawala kwa wema;
Atawafundisha
Mataifa haki yake,
Ajabu za pendo,
Ajabu za pendo,
Ajabu za pendo lake.