Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 161 PIGA PANDA nyimbo za wokovu
1
Piga panda na ya makelele;
Yesu yuaja tena!
Ipaze sauti, imba sana;
Yesu yuaja tena!
Anakuja, anakuja;
Yesu yuaja tena!
2
Itoe mwangwi sana vilima;
Yesu yuaja tena!
Yuaja kwa utukufu mwingi,
Yesu yuaja tena!
3
Itangazwe mahali po pote,
Yesu yuaja tena!
Mwokozi aliyetufilia,
Yesu yuaja tena!
4
Kuona machafuko twajua
Yesu yuaja tena!
Mataifa yakasiriana,
Yesu yuaja tena!
5
Maradhi, hofu hutuhubiri
Yesu yuaja tena!
Taabu, njaa hutulilia
Yesu yuaja tena!