Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 158 U MWENDO GANI NYUMBANI? nyimbo za wokovu
1
U mwendo gani nyumbani?
Mlinzi akanijibu,
Usiku sasa waisha,
Macheo karibu.
Usihuzunike tena,
Bali ulemee mwendo
Hata ushike, ufalme
Kule mwangani juu.
2
Na tena niliuliza,
Nchi yote akajibu:
Sasa mwendo watimika,
Milele karibu.
Usihuzunike tena,
Ishara kuu zasonga
Na viumbe vyangojea
Sauti ya Bwana.
3
Nikamwuliza shujaa,
Ndivyo kanitia moyo:
Shikilia mapigano,
Kitambo yaisha.
Usihuzunike tena,
Kazi ifanywe kwa moyo,
Tumeahidiwa tunu
Tuishapo shinda.
4
Siyo mbali na nyumbani!
Fikara tamu njiani.
Latupoza roho nalo,
Lafuta machozi
Usihuzunike tena,
Kitambo tutakutana
Wenye furaha kamili
Nyumbani mwa Baba.