Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 157 MFALME YU MLANGONI nyimbo za wokovu
1
Mfalme yu mlangoni,
Ndiye aliyetufia;
Mara wote wampendao
Atawakusanya.
Yuaja, yuaja,
Mlangoni anasimama;
Anakuja, anakuja,
Kuja kwake karibu.
2
Dalili za kuja kwake
Zinazidi kutimizwa
Karibuni wateule
Watamlaki Bwana.
3
‘Sitafute duniani
Amani wala furaha;
Mpaka Bwana arudi
Dhambi kuondoa.
4
Tutakaa na Mwokozi
Makaoni ya milele;
Daima tutafurahi
Kuwa watu wake.