Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 145 NAMTAKA BWANA YESU nyimbo za wokovu
1
Ulimwengu siutaki,
Namtaka Bwana Yesu;
Dunia hunidanganya;
Yesu yu mwaminifu.
Rehema ni ya ajabu!
Pendo bila kipimo!
Wokovu mkamilifu,
Amana ya uzima!
2
Ulimwengu siutaki,
Namtaka Bwana Yesu;
Kati ya dhoruba kali
Yeye wimbo mtamu.
3
Ulimwengu siutaki,
Namtaka Bwana Yesu;
Safarini duniani
Yeye furaha yangu.
4
Ulimwengu siutaki,
Namtaka Bwana Yesu;
Msalaba naamini,
Hata namwona Yesu.