Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 142 NASIKIA SAUTI YAKO nyimbo za wokovu
1
Nasikia mwito,
Ni sauti yako;
Nikasafiwe kwa damu
Ya kwangikwa kwako.
Nimesongea
Mtini pako,
Unisafi kwa damu
Ya kwangikwa kwako.
2
Ni mnyonge kweli,
Umenipa nguvu;
Ulivyonisafi taka
Ni utimilivu.
3
Yesu hunijuvya;
Mapenzi, imani,
Tumai, amani, radhi,
Hapa na Mbinguni.
4
Napata wokovu,
Wema na neema;
Kwako Bwana nina nguvu
Na haki daima.