Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 103 NJONI KWANGU nyimbo za wokovu
1
Yesu huita kwa upole mwingi,
atwita wewe nami;
Moyoni mwetu hungoja,
hukesha Hukungojea wewe.
Njoni kwangu, Mliochoka, njoni
Yesu huita kwa upole mwingi,
Akwita, Uje kwangu.
2
Atuombeapo usikawie,
Hutuombea sisi;
Usidharau wema na huruma,
Huruma kwetu sisi.
3
Siku za maisha hupita hima,
Hupita kwako, kwangu;
Usiku waja, kifo kinakuja,
huja kwako na kwangu.
4
Fikiri juu ya upendo wake,
upendo kwako, kwangu;
Dhambi zetu amekwisha samehe,
masamaha ni yetu.