Nyimbo Za Sifa
Wimbo 67 Yesu Atuchunga. Maneno ya wimbo
Yesu atuchunga
Mchunga wetu
Naye atufuta
Machozi yetu
Mkononi mwake
Hatuna hofu
Daima twapata
Kwake wokovu
Yesu atuchunga
Tumemjua
Na sauti yake
Twaitambua
Naye akituonya
Ni kwa upole
Tu kondoo zake
Hata milele
Yesu atuchunga
Aliwafia
Kondoo wakubwa
Na wana pia
Kwamba awajua
Kondoo zake
Hutiwa alama
Ya damu yake
Yesu atuchunga
Mikono yake
Imewaambata
Kondoo zake
Hapati wadhuru
Adui yule
Yesu awalinda
Hata milele