Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 50 MUNGU NAWE NANYI DAIMA nyimbo za wokovu
1
Mungu nawe nanyi daima;
hata twonane ya pili,
Awachunge kwa fadhili,
Mungu nawe nanyi daima.
Hata twonane juu,
hata twonane tena kwake;
Hata twonane juu,
Mungu nawe nanyi daima.
2
Mungu nawe nanyi daima;
awafunike mabawa,
Awalishe, awakuze;
Mungu nawe nanyi daima.
3
Mungu nawe nanyi daima;
kila wakati wa shida
Awalinde hifadhini;
Mungu nawe nanyi daima.
4
Mungu nawe nanyi daima;
awabariki na pendo
Ambalo halina mwisho;
Mungu nawe nanyi daima.