Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 19 MSALABANI PA MWOKOZI nyimbo za wokovu
1
Msalabani pa Mwokozi
Hapo niliomba upozi,
Moyo wangu ulitakaswa,
Na asifiwe.
Na asifiwe, Na asifiwe.
Alinikomboa kwa damu,
Na asifiwe.
2
Chini ya mti msumbufu
Niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu,
Na asifiwe.
3
Kwa ajabu ninaokoka,
Yesu anakaa moyoni;
Mtini alinifilia,
Na asifiwe.
4
Damu ya Yesu ya thamani
Huniokoa makosani;
Huniendesha wokovuni,
Na asifiwe.