Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 186 HATUTAAGANA TENA nyimbo za wokovu
1
Tuonapo na rafiki
Sote twafurahi,
Ila tumepaswa mwishowe
Kuagana tena.
Hatutaagana tena
Nyumbani mbinguni,
Kwenye nchi tamu juu,
Hatutaagana.
2
Twatumaini kwa furaha
Tutaonana juu
Na rafiki tulioaga
Tuishapo shinda.
3
Kule hatutatamka
Kamwe neno la kuaga,
Tutaimba daima
Tena nyimbo za furaha.