Nyimbo za wokovu
Wimbo 95 Kristo Mkombozi Alikufa Maneno ya wimbo
Kristo Mkombozi alikufa,
Kwa mwenye dhambi alimfia,
Jioshe na damu ya Kondoo,
Nitapita – pita juu yako.
Nionapo damu,
Nionapo damu;
Nionapo damu,
Nitapita – pita juu yako.
Mkuu wa waovu uje kwake,
Atimize ahadi zake;
Jioshe kisimani mwake,
Nitapita – pita juu yako Mtu yeyote atapata
Zawadi yake hukumuni;
Jifiche damuni mwa Kondoo,
Nitapita-pita juu yako.
Uaminifu wa ajabu,
Huruma tele na upendo;
Upate amani kwa damu,
Nitapita-pita juu yako.