Nyimbo za wokovu
Wimbo 79 Fanyeni Kazi Zenu Maneno ya wimbo
Fanyeni kazi zenu,
Usiku si mbali;
Kesheni saa zenu
Mkastahimili;
Kwa Yesu tumikeni
Na hiyo injili,
Sana wahubirini
Watu wa Mbali.
Fanyeni kazi zenu
Giza yasongea;
Na wengi wenziwenu
Hawajasikia;
Msipoteze moja
Dakika ni hizi;
Bwana atarejea
Mwisho wa kazi.
Fanyeni kazi zenu,
Hivi jua latwa;
Wote walio kwenu
Mungu huwapenda;
Basi tumjuaye
Na tuwafundishe
Ili Yesu ajaye
Tumfurahishe.