Nyimbo za wokovu
Wimbo 73 Ushirika Mkuu, Furaha Yangu Maneno ya wimbo
Ushirika mkuu, furaha yangu
Kumtegemea Bwana Yesu,
Nina baraka, amani pia,
Kumtegemea Bwana Yesu.
Raha, Raha,
Nina raha na salama,
Raha, Raha,
kwa kumtegemea Yesu.
Ni halisi kutembea naey,
Kwa kumtegemea Yesu.
Naona nuru njiani mwangu,
Kumtegemea Bwana Yesu.
Sioni shaka wala hasara,
Kumtegemea Bwana Yesu;
Nina amani kwake Mwokozi,
Kumtegemea Bwana Yesu.