Nyimbo za wokovu
Wimbo 69 Nyimbo Na Tuziimbe Tena Maneno ya wimbo
Nyimbo na tuziimbe tena
Za alivyotupenda mbele;
Kwa damu ya thamani sana!
Mbinguni hwonana milele.
Twonane milele,
Twonane bandarini kule;
Twonane milele,
Twonane bandarini kule.
Hupozwa kila aoshwaye
Kwa damu ya Kondoo yule;
Ataishi afurahiye
Vya Yesu mbinguni milele.
Hata sasa hufurahia
Tamu yake mapenzi yale,
Je, kwake tukifikilia,
Kutofarikana milele?
Twende mbele kwa Jina lake,
Hata aje Yesu ye yule,
Atatukaribisha kwake,
Tutawale naye milele.
Na beramu tuikunjue
Kumsifu Mwokozi yule,
Ili watu wote wajue
Wokovu u kwake milele.