Nyimbo za wokovu
Wimbo 66 Neno Lake Yesu Maneno ya wimbo
Neno lake Yesu, na ahadi
Zimepita jumbe zote duniani,
Kristo Mtakatifu, hana dhambi,
Yeye ni Kielelezo kwangu mimi.
Ninapoongozwa,
Na Yesu Bwana;
Ninapoongozwa,
Kweli, nitamwandama.
Pendo lake Yesu, naliona,
Lashinda pendo zozote za dunia;
Yesu Mwaminifu, huokoa,
Yeye ni Kielelezo kwangu sasa.
Yesu anasema, Uje kwangu,
Ulemewaye upate raha yangu;
Amini ahadi zake Bwana,
Mtegemee Mwokozi kwa salama.