Nyimbo za wokovu
Wimbo 56 Mbele Ninaendelea Maneno ya wimbo
Mbele ninaendelea,
Ninazidi kutembea;
Maombi uyasikie,
Ee Bwana, unipandishe.
Ee, Bwana, uniinue,
Kwa imani nisimame;
Nipande milima yote,
Ee Bwana, unipandishe.
Sina tamani nikae,
Ni mahali pa shaka, kamwe;
Hapo wengi wanakaa,
Kuendelea naomba.
Nisikae duniani,
Ni mahali pa Shetani;
Natazamia mbinguni,
Nitafika na imani.
Nataka nipandishwe juu,
Zaidi yale mawingu;
Nitaomba nifikishwe,
Ee Bwana, unipandishe.