Nyimbo za wokovu
Wimbo 5 Kwa Yote Aliyotenda Maneno ya wimbo
Kwa yote aliyotenda,
Sitaacha kumsifu,
Neema yake imetosha,
Sitaacha kumsifu.
Sitaacha kumsifu,
Mwokozi, Mwokozi;
Sitaacha kumsifu Aliye Mkombozi.
Anipaye nguvu zake,
Sitaacha kumsifu,
Nitembee njia yake,
Sitaacha kumsifu.
Hunipa wokozi wake,
Sitaacha kumsifu,
Kwa kunipa nguvu zake,
Sitaacha kumsifu.
Ninaposafiri hapa,
Sitaacha kumsifu,
Nitakapofika mbingu,
Sitaacha kumsifu.