Nyimbo za wokovu
Wimbo 22 Nina Haja Nawe Maneno ya wimbo
Nina haja nawe
Kila saa;
Hawezi mwingine
Kunifaa.
Yesu nakuhitaji
Vivyo kila saa!
Niwezeshe mwokozi,
nakujia.
Nina haja nawe;
Kaa nami,
Na maonjo haya,
Hayaumi.
Nina haja nawe,
Kila hali,
Maisha ni bure,
Uli mbali.
Nina haja nawe;
Nifundishe,
Na ahadi zako Zifikishe.
Nina haja nawe;
Mweza yote,
Ni wako kabisa
Siku zote.