Nyimbo za wokovu
Wimbo 205 Rafiki Zangu Wanatafuta Maneno ya wimbo
Rafiki zangu wanatafuta
Vile vileteavyo furaha;
Naijua siri kuvipata,
Katika Yesu tuna anasa.
Haja yangu ni kwa Yesu,
Aridhisha kwa furaha;
Bila Yeye sitafaa,
Ndaniyake uzima.
Wengine huishika mizigo
Zinazolemeza na kilio;
Bali tunaye Rafiki Mwema,
Atakayesaidia sasa.
Maskini wote wanamhitaji,
Waondoke kutoka dhambini;
Yesu atawaokoa kweli,
Ili sasa wapate kuishi.