Nyimbo za wokovu
Wimbo 202 Alishuka Kutoka Mbinguni Maneno ya wimbo
Alishuka kutoka mbinguni,
Yesu Bwana wangu;
Kwangu akaziondoa dhambi,
Napendwa na Mungu.
Sina budi kumpenda,
Yesu Mwokozi,
Sina budi kumpenda,
Ndiye Mwokozi.
Sistahili kupata neema,
Neema yake mkuu;
Na badala yangu akateswa,
Kwa uovu wangu.
Yesu yu Mwema kuliko wote,
Hupenda kwa haki;
Nauona utukufu wake,
Na Mungu mbinguni.