Nyimbo za wokovu
Wimbo 183 Kwa Damu Ya Yesu Naokoka Maneno ya wimbo
Kwa damu ya Yesu naokoka!
Nikageuka niwe mtu mpya;
Baba asifiwe na Mwana pia,
Kwa damu ya Yesu naokoka.
Naokoka! Naokoka!
Dhambi zangu zote zaondolewa;
Naokoka! Naokoka!
Naokolewa na damu yake Bwana.
Kwa damu ya Yesu naokoka!
Malaika wafurahi kuona;
Ni Mwana wa Baba mrihti wa Mwana,
Kwa damu ya Yesu naokoka.
Kwa damu ya Yesu naokoka!
Mapenzi ya Baba ya imetendeka;
Alinunua na gharama kubwa.
Kwa damu ya Yesu naokoka.
Kwa damu ya Yesu naokoka,
Asifiwe Baba na Mwana pia;
Roho asifiwe huleta raha,
Kwa damu ya Yesu naokoka.