Nyimbo za wokovu
Wimbo 174 Namhitaji Yesu Maneno ya wimbo
Namhitaji, namhitaji Yesu,
Hakuna rafiki kama Mungu;
Nmhitaji, hayo naungama,
Siwezi kuchukua mzigo bila Bwana.
Namhitaji, Bwana Yesu,
Namhitaji kila saa;
Namhitaji mwangani,
Na hata mawinguni,
Njiani kila siku, Ee, namhitaji.
Namhitaji, namhitaji Yesu,
Aziongoze hatua zangu;
Namhitaji, adui washindwe,
Kushinda pasipo Yesu siwezi kwamwe.
Namhitaji, namhitaji Yesu,
Yu rafiki wa wenye halifu;
Namhitaji, Yesu anitosha,
Yu mwaminifu na Mwema, hufurahisha.