Nyimbo za wokovu
Wimbo 172 Sijui Sababu Ya Neema Maneno ya wimbo
Sijui sababu ya neema
Niliopewa na Mungu,
Sikulistahili pendo lake,
Wala wokovu wa Yesu.
Namjua niliyemwamini,
Na kusadiki kwamba waweza
Kulinda kilichowekwa
Amana kwake Bwana.
Sijui jinsi nilivyopewa
Imani ya kumwamini,
Neno lake Yesu lilileta
Amani yake moyoni.
Sijui jinsi Roho wa Mungu
Awaonyeshavyo watu,
Wapate kuzitambua dhambi,
Na kumfuata Yesu.
Sijui kama mambo yajayo
Yatakuwa ya salama,
Lakini nitamwamini Yesu
Mpaka tutaonana.
Sijui siku gani ya Bwana
Hapa atakaporudi,
Nitamngojea na imani
Hata kumlaki hewani.