Nyimbo za wokovu
Wimbo 171 Sijui Ilipotoka Maneno ya wimbo
Sijui ilipotoka,
Amani moyoni;
Bali najua najazwa
Na raha moyoni.
Ni amani moyoni mwangu,
Ni amani moyoni mwangu;
Ijapo dhambi ziko karibu,
Kristo Yuko, Hudumu.
Kwa mambo ya maishani
sitafadhaika,
Nikilemewa kazini
Sitahuzunika.
Sijui juu ya upendo
Jinsi ukuwavyo,
Umenifufusha roho
Kufurahi nao.
Sistahili kifo chake
Wala ukombozi,
Ningeteswa hapa naye,
Naye ningerithi.