Nyimbo za wokovu
Wimbo 17 Nilipoona Chemchemi Maneno ya wimbo
Nilipoona chemchemi,
Kwa dhambi zangu zote;
Nikasikia sauti
Kusema, Uwe safi.
Nitamsifu, nitamsifu,
Msifuni Mwana – Kondoo;
Mpeni sifa za moyo,
Kwani hutupa utakaso.
Njia yake ni nyembamba,
Vyote navimtolea;
Fahari na tumaini
Hayo nimeondoa.
Moyo wangu ulichomwa,
Kwa moto wake Mungu;
Sitakosa kumsifu,
Bwana wa utukufu.
Jina la Yesu ni heri,
Aliyenikubali;
Amezisamehe dhambi,
Tena hunifadhili.
Utukufu kwake Baba,
Utukufu Kwa Mwana;
Utukufu naye roho,
Utatu ndani Mmoja