Nyimbo za wokovu
Wimbo 162 Katika Nchi Nyingi Maneno ya wimbo
Katika nchi nyingi
Wako watoto wengi
Wasiosikia habari njema;
Kristo aliwafia
Na aliwanunua,
Sasa wanangoja kukaribishwa.
Yesu hupenda watoto,
Wote ulimwenguni;
Weupe na weusi,
Kwake ni wa thamani,
Yesu awapenda watoto wote.
Sauti twasikia,
Na wanatulilia,
Nani atakayewasaidia?
Hawa wenye thamani
Kwake Yesu Mwokozi,
Mkononi mwa Yesu tutawaweka.
Kutoka mbali sana,
Waje kubarikiwa
Watoto hawa ndio wa thamani;
Tumtii Bwana,
Tutapata kipawa,
Atakaporudi toka mbinguni.